Thursday, April 30, 2009

mwili wa maira wawasili











Marehemu Moses Maira (Kushoto)Mwili wa wakili maarufu Moses Maira unatarajiwa kuwasili nchini leo usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi, KLM. Kwa mujibu wa wakili mwenzake, Mabere Marando, baada ya mwili huo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam saa 6 usiku, utapelekwa nyumbani kwake Tabata. Kesho kutwa asubuhi, mwili utachukuliwa hadi Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni kwa ajili ya ibada maalumu kabla ya kupelekwa katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya heshima za mwisho. Baada ya hapo, Marando alisema, msafara wa kwenda katika makaburi ya Kinondoni kwa maziko utaanza ambapo anatarajiwa kuzikwa saa 9 alasiri. Maira (66) alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita mjini Houston, Texas, Marekani, alikokwenda kutibiwa ugonjwa wa moyo na kisukari. Kabla ya safari yake ya Marekani, Maira alikuwa akimtetea aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Abdallah Zombe, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Dar es Salaam.Habari Kwa Hisani: Habarileo

Jiji la Dar es Saalam na vitongoji vyake, jana lilizizima kwa mishindo mkubwa na mitetemo ya mabomu na makombora yaliyolipuka kwa kupishana kutoka katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 671 Mbagala.
Mtafaruku huo, pia uliyakumba maeneo jirani na kusababuisha vifo vya watu, mamia kujeruhiwa, nyumba kuungua, huku watoto 200 wakipotezana na familia zao.Mamia ya wakazi wa jiji hilo hasa Mbagala na vitongoji vyake walionekana kuchanganyikiwa walikuwa wakihangaika kukimbia nyumba zao kwa lengo la kujiokoa.
Katika harakati za kujiokoa baadhi ya wananchi ho walitumbukia mtoni huku baadhi yao wakiwasahau watoto wao na vikongwe nyumba bila msaada wowoteBarabara ya Kilwa kuanzia eneo la uwanja wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, Kambi ya Jeshi ya Twalipo hadi Mbagala Kizuiani ilipo kambi hiyo ya kikosi cha 671, ilijaa askari wa JWTZ waliojipanga kando na kuongoza magari, huku wakizuia mengine kuelekea karibu na eneo la tukio.
Majira ya saa tano asubuhi mshindo mzito wa kwanza ulisikika na ambao ulitikisa takriban majengo yote katikati ya jiji, huku moshi mweusi ukionekana angani upenda wa barabara ya Kilwa na dakika chache baadaye magari ya vikosi vya zima moto, polisi, JWTZ na waandishi wa habari vilihangaika kuelekea kwenye tukio.Hata hivyo misafara hiyo ilikwamishwa njiani na msururu mrefu wa magari na wananchi waliokuwa wakikimbia kutoka eneo karibu na tukio kuelekea katikati ya jiji, hivyo kulazimika kutafuta njia nyingine ya kufika eneo la tukio.
Vikosi vya zima moto viliwahi eneo la tukio, huku milipuko ilikuwa ikiendelea kwa mpishano wa dakika kati ya tatu na sita majira ya asubuhi na saa za jioni ilipugua kwa mpshano wa robo saa hadi dakika 20.Habari Na Picha Kwa Hisani: charahani














Tuesday, April 28, 2009

waziri mkuu akutana na viongozi wa dini balibali


waziri mkuu mhimiwa pinada akutana na viongozi wa dini balibali na kufanya maongrzi nao leo dodoma

Monday, April 20, 2009