Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaambia Watanzania kuwa uhuru wa watu kusema ambao umeshamiri nchini kwa sasa siyo uhuru wa watu kutukana.Rais pia amesisitiza kuwa uhuru wa kusema wa mtu mmoja unaishia pale unapoanza uhuru wa mtu mwingine.Rais Kikwete ameyasema haya leo, Jumanne, Mei 19, 2009, wakati alipokutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi katika eneo la Kusini mwa Jimbo la California baada ya kuwa amewasili mjini Los Angeles, akitokea mjini San Francisco, ambako alianzia ziara yake ya Marekani mwishoni mwa wiki.Akiwaelezea Watanzania hao kuhusu hali ya kisiasa nchini, Rais Kikwete amesema kuwa nchi ni shwari na tulivu, na kuwa uhuru wa watu kusema unashamiri sana nchini kwa sasa.“Watu siku hizi wanasema sana, na wakati mwingine wengine wanapitiliza mipaka na kuanza kutukana, kwa kuamini kuwa uhuru wa kusema ni tiketi ya kutukana. Sisi katika Serikali tunavumilia hali hiyo kwa sababu tunaamini kuwa hali hiyo ni uchanga tu wa demokrasia na watu kutokuzoea uhuru huu wa kusema,” amesema Rais Kikwete.Ameongeza kuwa itafika wakati watu hao ambao wanachanganya uhuru wa kusema na matusi watakuwa na ukomavu wa kutosha na hivyo kuuzoea uhuru huo.Kuhusu suala la kutungwa kwa sheria inayotoa uhuru kwa Mtanzania, anayetaka, kuwa raia wa nchi mbili, Rais Kiwete amesema kuwa Serikali haijaenda mbali na suala hilo kwa sababu hoja hiyo haikupokelewa vizuri nchini wakati ilipozunguzwa kwa mara ya kwanza.“Iko, nadhani, hoja ya msingi ya kuanzishwa kwa taratibu hiyo, lakini ukweli ni kwamba hoja hiyo bado haikubaliki kwa baadhi ya wenzenu huko nyumbani. Bado hoja hiyo inakabiliwa na resistance (upinzani),” amesema Rais Kikwete na kuongeza:“Hata hivyo, tutaendelea kuelimishana na kushawishiana kuhusu suala hili. Kama nilivyosema hoja hiyo haikupokelewa vizuri na baadhi ya watu ilipojitokeza kwa mara ya kwanza.”Hoja ya uraia wa nchi mbili ni hoja inayosukumwa kweli kweli na Watanzania wanaoishi nje, na Rais Kikwete aliulizwa swali kuhusu suala hilo hilo wakati alipowasili mjini San Francisco kuanza ziara ya siku nane katika Marekani Jumapili iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hello... hapi blogging... have a nice day! just visiting here....
ReplyDelete