Thursday, May 21, 2009

ziara ya rais jk marekani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaambia Watanzania kuwa uhuru wa watu kusema ambao umeshamiri nchini kwa sasa siyo uhuru wa watu kutukana.Rais pia amesisitiza kuwa uhuru wa kusema wa mtu mmoja unaishia pale unapoanza uhuru wa mtu mwingine.Rais Kikwete ameyasema haya leo, Jumanne, Mei 19, 2009, wakati alipokutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi katika eneo la Kusini mwa Jimbo la California baada ya kuwa amewasili mjini Los Angeles, akitokea mjini San Francisco, ambako alianzia ziara yake ya Marekani mwishoni mwa wiki.Akiwaelezea Watanzania hao kuhusu hali ya kisiasa nchini, Rais Kikwete amesema kuwa nchi ni shwari na tulivu, na kuwa uhuru wa watu kusema unashamiri sana nchini kwa sasa.“Watu siku hizi wanasema sana, na wakati mwingine wengine wanapitiliza mipaka na kuanza kutukana, kwa kuamini kuwa uhuru wa kusema ni tiketi ya kutukana. Sisi katika Serikali tunavumilia hali hiyo kwa sababu tunaamini kuwa hali hiyo ni uchanga tu wa demokrasia na watu kutokuzoea uhuru huu wa kusema,” amesema Rais Kikwete.Ameongeza kuwa itafika wakati watu hao ambao wanachanganya uhuru wa kusema na matusi watakuwa na ukomavu wa kutosha na hivyo kuuzoea uhuru huo.Kuhusu suala la kutungwa kwa sheria inayotoa uhuru kwa Mtanzania, anayetaka, kuwa raia wa nchi mbili, Rais Kiwete amesema kuwa Serikali haijaenda mbali na suala hilo kwa sababu hoja hiyo haikupokelewa vizuri nchini wakati ilipozunguzwa kwa mara ya kwanza.“Iko, nadhani, hoja ya msingi ya kuanzishwa kwa taratibu hiyo, lakini ukweli ni kwamba hoja hiyo bado haikubaliki kwa baadhi ya wenzenu huko nyumbani. Bado hoja hiyo inakabiliwa na resistance (upinzani),” amesema Rais Kikwete na kuongeza:“Hata hivyo, tutaendelea kuelimishana na kushawishiana kuhusu suala hili. Kama nilivyosema hoja hiyo haikupokelewa vizuri na baadhi ya watu ilipojitokeza kwa mara ya kwanza.”Hoja ya uraia wa nchi mbili ni hoja inayosukumwa kweli kweli na Watanzania wanaoishi nje, na Rais Kikwete aliulizwa swali kuhusu suala hilo hilo wakati alipowasili mjini San Francisco kuanza ziara ya siku nane katika Marekani Jumapili iliyopita.








hapa alipo tembelea google na kupata maelezo kadha wa kadha




Tuesday, May 19, 2009

kesi ya kina mramba ya futwa







huyu ndiye mwanasheria machachari anae watetea wa kina mramba na na julikana kwa jina la prof, leonard shahidi ameweza kuleta upinzani mkwali kwa jupo la wanasheria wa serikali



Thursday, May 7, 2009

president kikwete visit ,denmark and south africa


President Jakaya Mrisho Kikwete has left the country for Denmark and South Africa on official visits. According to a statement issued yesterday by the State House in Dar es Salaam, President Kikwete left on Monday night by KLM to Denmark, where he was expected to attend a three-day meeting of the Denmark-Africa Commission scheduled to kick off today. President Kikwete is a member of the commission which is chaired by Danish Prime Minister Anders Fogh Rasmussen. Youth and employment in Africa would be among key topics expected to feature in the meeting. The meeting will also work on the commission`s last report. President Kikwete is also scheduled to hold talks with Danish Shipowners` Association chairman Peter Bjerre-gaard. According to the schedule, President Kikwete would leave Denmark on Thursday for South Africa, where he will attend the swearing-in of presidential candidate Jacob Zuma, following his party\'s victory in the April 22 general elections.

Thursday, April 30, 2009

mwili wa maira wawasili











Marehemu Moses Maira (Kushoto)Mwili wa wakili maarufu Moses Maira unatarajiwa kuwasili nchini leo usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi, KLM. Kwa mujibu wa wakili mwenzake, Mabere Marando, baada ya mwili huo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam saa 6 usiku, utapelekwa nyumbani kwake Tabata. Kesho kutwa asubuhi, mwili utachukuliwa hadi Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni kwa ajili ya ibada maalumu kabla ya kupelekwa katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya heshima za mwisho. Baada ya hapo, Marando alisema, msafara wa kwenda katika makaburi ya Kinondoni kwa maziko utaanza ambapo anatarajiwa kuzikwa saa 9 alasiri. Maira (66) alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita mjini Houston, Texas, Marekani, alikokwenda kutibiwa ugonjwa wa moyo na kisukari. Kabla ya safari yake ya Marekani, Maira alikuwa akimtetea aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Abdallah Zombe, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Dar es Salaam.Habari Kwa Hisani: Habarileo

Jiji la Dar es Saalam na vitongoji vyake, jana lilizizima kwa mishindo mkubwa na mitetemo ya mabomu na makombora yaliyolipuka kwa kupishana kutoka katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 671 Mbagala.
Mtafaruku huo, pia uliyakumba maeneo jirani na kusababuisha vifo vya watu, mamia kujeruhiwa, nyumba kuungua, huku watoto 200 wakipotezana na familia zao.Mamia ya wakazi wa jiji hilo hasa Mbagala na vitongoji vyake walionekana kuchanganyikiwa walikuwa wakihangaika kukimbia nyumba zao kwa lengo la kujiokoa.
Katika harakati za kujiokoa baadhi ya wananchi ho walitumbukia mtoni huku baadhi yao wakiwasahau watoto wao na vikongwe nyumba bila msaada wowoteBarabara ya Kilwa kuanzia eneo la uwanja wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, Kambi ya Jeshi ya Twalipo hadi Mbagala Kizuiani ilipo kambi hiyo ya kikosi cha 671, ilijaa askari wa JWTZ waliojipanga kando na kuongoza magari, huku wakizuia mengine kuelekea karibu na eneo la tukio.
Majira ya saa tano asubuhi mshindo mzito wa kwanza ulisikika na ambao ulitikisa takriban majengo yote katikati ya jiji, huku moshi mweusi ukionekana angani upenda wa barabara ya Kilwa na dakika chache baadaye magari ya vikosi vya zima moto, polisi, JWTZ na waandishi wa habari vilihangaika kuelekea kwenye tukio.Hata hivyo misafara hiyo ilikwamishwa njiani na msururu mrefu wa magari na wananchi waliokuwa wakikimbia kutoka eneo karibu na tukio kuelekea katikati ya jiji, hivyo kulazimika kutafuta njia nyingine ya kufika eneo la tukio.
Vikosi vya zima moto viliwahi eneo la tukio, huku milipuko ilikuwa ikiendelea kwa mpishano wa dakika kati ya tatu na sita majira ya asubuhi na saa za jioni ilipugua kwa mpshano wa robo saa hadi dakika 20.Habari Na Picha Kwa Hisani: charahani














Tuesday, April 28, 2009

waziri mkuu akutana na viongozi wa dini balibali


waziri mkuu mhimiwa pinada akutana na viongozi wa dini balibali na kufanya maongrzi nao leo dodoma

Monday, April 20, 2009

Tuesday, March 31, 2009

Tanzania kupeleka jeshi la kulinda amani Darfur mwezi ujao

msuluhishi wa mgogoro darfur DR .Salim Ahmed Salim akiwaaga wanajeshi wa tanzania watakao enda kulinda amani Darfur.. pembenni akiwa na mnadhimu mkuu wa jwtz Adulraman shimbo





msuluhishi wa mgogoro wa Darfur akiagana na kamanada wa kikosi kitakacho enda darfur kulinda usalama luteni kanali Ally katimbe leo

jk na mama salma wameremeta miaka 20 ya ndoa


ilikua full shangwe wakati jk akikata keki iliyo kua imeandaliwa kwajili ya kusherekea miaka 20 ya ndoa ........... undugu.blogspot.com na crew zima inatoa pongezi za dhati kwako mheshimiwa kikwete pamoja na mama salma kikwete

jk Amkaribisha Governor Genaral wa Australia ikulu






Monday, March 30, 2009

Governor General wa Auatralia atua bongo


makamu wa raisi akimlaki gonernor general wa australia Quentin Bryce katika uwanja wa mwalimu julius kambarage nyerere tayari kwa ziara ya siku tatu nchini

mh chenge apandishwa mahakamani mchana huu







mtuhumiwa wa kesi ya kugonga na kua mh chenge apandishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili juu ya ajali iliyotokea

Ajali mbaya ya treni yatokea dodoma na kusababisha vifo vya watu kumi 13







jk audhuria mkutano wa sadac uliyo fanyika swaziland

viongozi walioudhuria mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyezi wao mfalme wa swaziland


jk hapa akiongea na raisi wa madagascar aliye ondolewa madarakani mh marc ravalomanana

jk ampongeza anne kilango[mb] kwa kunyakua tuzo

anne kilango malecela akikabidhiwa tunzo ya mwanamke jasiri tanzania na kaimu wa ubalozi wa marekani nchini bw larry Andrie


Sunday, March 29, 2009

kumbukumbu kutoka maktaba


siku ya kumbukumbu baada ya kuapishwa kwa raisi JK akiwa na viongozi walio udhuria inaguration ceremony

Saturday, March 28, 2009

mheshimiwa chenge katika msukosuko wa ajali yake


mh chenge akitoa maelezo kwa kwa naibu mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai afande peter kivuyo na kamada wa traffic dar afande mohamed mpinga kuhusu jinsi ajali yake ilivyo tokea